Kupata VVU inaweza isiwe hukumu ya kifo, lakini madhara yake bado ni makubwa. Watu wengi wanaoishi na VVU wanakabiliwa na ukanaji na kutokuwa na hakika kuhusu mustakabali wao, na wasiwasi huu unaweza kuonekana kwa undani zaidi kwa watoto na vijana. Kivuko na Watoto kinawapa mashirika na watu binafsi kitabu ambacho wanaweza kukitumia kuwahusisha watoto walioathirika kwa VVU na walezi wao, kwa kutumia mazoezi yenye uwezo mkubwa wa kuwasilisha taarifa, kuchunguza kanuni, kugundua uwezo wao, na kila mtu binafsi na kwa pamoja kuunda njia madhubuti za ustawi. Vipindi vya mafunzo vinajumuisha mada nyingi kwa kuzingatia mfumo wa haki za mtoto na jinsia ikiwa ni pamoja na ustawi wa kisaikolojia na kijamii na uimara, uthubutu, ukiwa, upimaji wa VVU, kuishi vizuri na VVU, kuzuia unyanyasaji wa kijinsia, na kuwasaidia walionusurika na unyanyasaji. Vinashughulika na masuala yanayowakabili vijana wanaokua, ambayo kwa hakika yanaweza kuwa na changamoto kwa wale walioathirika kwa VVU - kuanzia urafiki shuleni, hadi katika uhusiano, ujinsia, na njia za kujipatia riziki. Kila kipindi kati ya vipindi hivi kinaeleza kwa uwazi madhumuni yake makubwa, na kuweka lengo na njia kwa kila shughuli. Shughuli nyingi zinatekelezwa na washirikikwa kushirikiana na makundi rika yao matatu tofauti ya watoto wadogo (umri wa miaka 5-8), na watoto wakubwa (umri wa miaka 9-14) na walezi. Wakati mwinigine kila kundi rika hufanyakazi katika makundi madogo madogo ya jinsi. Makundi rika hayo wakati mwingine hufanya kazi pamoja, au kujumuika pamoja kushrikishana walichojifunza na kujadili njia zingine za kuhusiana. ?NOTE not for sale from this publisher in Uganda and Tanzania
ThriftBooks sells millions of used books at the lowest everyday prices. We personally assess every book's quality and offer rare, out-of-print treasures. We deliver the joy of reading in recyclable packaging with free standard shipping on US orders over $15. ThriftBooks.com. Read more. Spend less.